HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI ILIOANDALIWA NA KINANA KWA AJILI YA KIONGOZI WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA VIETNAM MJINI DODOMA JANA SEPTEMBER 21,2017.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Alhaj Adamu Kimbisa akimtolea ufafanuzi wa zawadi ya kinyango Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam uku katibu Mkuu wa (CCM) akishuhudia zoezi hilo,wakati wa hafla ya Chakula cha Jion ilioandaliwa na kinana.
 Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Comred Abdurahman Kinana akizungumza kabla ya Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam kukabidhiwa zawadi na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Alhaj Adamu Kimbisa wakati wa hafla ya Chakula cha Jion.
 Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Comred Abdurahman Kinana akizungumza na balozi wa Vietnam Nguyen kim Doanh.
 Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Comred Abdurahman Kinana akifurahia jambo na wageni wake toka chama cha Kikomunisti cha Vietnam (VCP) jana wakati wa hafla ya chakula cha jion.
 Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Comred Abdurahman Kinana akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jion.
 Wajumbe wa Chama cha kikomunisti cha Vietnam (VCP) pamoja na Katibu mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazaza CCM wa (pili toka kushoto) wakifuatilia mazungumzo ya Katibu mkuu wa CCM  katika hafla ya chakula cha jion.
Baadhi Wajumbe wa Sekretariet wakifuatilia mazungumzo ya Katibu mkuu wa CCM  katika hafla ya chakula cha jion.
 Katibu Mkuu wa CCM Comred Abdurahman Kinana na Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam wakinyanyua glasi kabla ya kuzigonganisha kutakiana heri kabla ya chakula cha jion alicho mwandalia Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam Mjini dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Alhaj Juma Kimbisa pamoja na Katibu wa idara ya SUKI kanal mstaaf Ngemela Rubiga wakinyanyua glasi kabla ya kuzigonganisha kutakiana heri kabla ya chakula cha jion  Katibu mkuu wa CCM alicho mwandalia Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam Mjini dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar DKT.Abdallah Mabodi akiagana na Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam mara baada ya kumalizika hafla ya chakula cha Usiku ilioandaliwa na Katibu mkuu wa CCM Comred Abdulrahman kinana Mjini dodoma.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Comred Abdulrahman Kinana akiagana na Mgeni wake Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam mara baada ya kumalizika kwa hafla ya chakula cha jion aliomwandalia mgeni wake   Mjini dodoma. (PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)fahadin siraji

Posted in

Spread the love

WAWILI JELA MIAKA 22 KILA MMOJA KWA DAWA ZA KULEVYA


Na Mwandishi Maalum
Abbas Kondo Gede na  Albeto Mandes wamehukumiwa kwenda jela miaka 22 kila moja kwa  kosa la   kujihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya Cocaine na Heroin.

Washitakiwa hao ambao walitenda makosa yao kwa nyakati tofauti wamehukumiwa pia kulipa faini ya jumla ya  shilingi  320.7 milioni.

                Hukumu  ya Abbas Kondo  Gede   ya kwenda jela  miaka 22 na  kulipa faini ya  jumla ya shilingi  175,764,000/=  imetolewa  leo  (  Jumatano)   na   Mhe. Jaji   Korosso baada  ya kujiridhisha  pasipo shaka kwamba, mshtakiwa alikuwa na   hatia ya kujihusisha na  biashara ya dawa za kulevya.

Abbas Kondo Gede  mtanzania, na  mkazi wa  mtaa wa Lindi, Wilaya ya  Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam, na ambaye  alikuwa ni mcheza mpira wa miguu.  Alikamatwa tarehe 14/5/2011 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akitokea  Sao Paulo, Brazil,  kwa usafiri wa  Shirika la  Ndege la Quater akiwa na   kete 77 sawa na  gramu 1,171.75  za   cocaine   zilizokuwa na thamani  ya   shilingi  58,588.000/= milioni.

Kesi ya  Abbas Gede iliendeshwa na   Mawakili wa Serikali  Batilda Mushi na Frank Tawala ambapo katika  maelezo yao waliiomba Mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine wanaojihusisha na  biashara hiyo haramu.
 Kwa upande wa  Albeto Mendes ambaye ni  raia wa Guinea  Besau yeye alikamatwa  tarehe 15/4/2012 katika  Uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage  Nyerere akiwa na    gram 1,277.41 za Heroine  zilizokuwa na thamani ya   shilingi  milioni  57,483.000/= akiwa katika harakati  za kusafiri   kwenda  nchini Mali.
 Hukumu ya Albeto  Mendes  ya kwenda jela miaka 22 na kulipa faini  ya shilingi  144,955,700/= imetolewa leo  ( jumatano) na Mhe.  Jaji Mfawidhi Matogolo baada ya  kujiridhisha pasipo shaka kwamba mshtakiwa alikuwa na hatia.
 Mawakili wa Serikali  walioendesha kesi hiyo na kuiomba  Mahakama kutoa  adhabu kali  walikuwa ni    Joseph Maugo ambaye ni  Wakili wa Serikali  Mwandamizi na  Wakili  Clara Chalwe.
Imetolewa na
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Dar es Salaam
20/9/2017


Bashir Nkoromo

Posted in

Spread the love

SEKRETARIETI YA CCM CHINI YA KINANA YAFANYA MAZUNGUMZO NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA VIETNAM MJINI DODOMA, LEO

 Katibu Mkuu wa CCM abdulrahman Kinana akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Chau Van Lam alipoasili kwa ajili ya mazungumzo na Sekretarieti ya CCM chini ya Kinana, leo katika ukumbi wa Kamati Kuu ya CCM, ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete nje kidogo ya mji wa Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-zanzibar Jumanne Mabodi. Katikati ni katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.
 Kiongozi huyo akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Jumanne Mabodi
 Kiongozi huyo akiendelea kusalimia viongzi wa CCM
 Kiongozi huyo akiendelea kusalimia viongozi wa CCM
 Kiongozi huyo akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka
 Kiongozi huyo akimsalimia Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi ya CCM
 Kinana akimpeleka mgeni wake eneo la kufanyia mazungumzo
 Mazungumzo yakianza
 Mazungumzo yakiendelea
 Mazungumzo yakiendelea
 Kinana akitambulisha ujumbe wake kwa mgeni
 Katibu wa CCM mkoa wa Dodoma akizungumza na mwandishi wa Uhuru Fm aliyekuwa akifuatilia mazungumzo hayo
 Ujumbe wa CCM kwenye mazungumzo hayo
 Chau akimpa zawadi Kinana baada ya mazungumzo hayo
 Kinana akimshukuru kwa zawadi mgeni huyo
 Chau akimpa zawadi nyinyine Kinana
 Chau akimpa zawadi ya Kitabu cha misingi ya Kimunisti cha Veitnam, Kinana
 Chau akizawadia Kinana tarumpeta la kisili ya Veitnam
 Kabla ya kumkabidhi akaliungurumisha kidogo
 Kinana akaipokea zawadi
 Kisha Kinana akaonyeshwa kidogo namna ya kuliungurumisha
 Kisha akalipuliza kwa uhodari
 Kinana akapewa zawadi ya kofia ya asili ya Kivietnam
 Akaipokea kwa furaha kofia hiyo
 Kisha akaivaa kofia hiyo akiifurahia 
 Akaendelea kuifurahia kofia hiyo 
 Kinana akajibu mapigo na yeye kwa kumpa zawadi ya picha maridhawa ya kuchorwa
 Chau akaipokea zawadi hiyo kwa furaha
 Kinana akimweleza Chau undani wa picha hiyo
 Kisha ikapigwa picha ya pamoja 
 Kinana akaagana na mgeni wake
 Kinana akimsindikiza mgeni wake baada ya mazungumzo hayo 
 Ngemela akizungumza na waandishi kuwajulisha kilichojiri kwenye mazungumzo hayo
ZIFUATAZO NI PICHA ZA MAPOKEZI CHAU ALIPOWASILI DODOMABashir Nkoromo

Posted in

Spread the love